

Lugha Nyingine
诺诺助手(诺诺助手客户端下载)V3.1.0.1官方版
![]() |
Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania (wa tatu toka kulia) na wageni wengine wakishiriki kwenye hafla ya kukata utepe wa EACLC mjini Dar es Salaam, Tanzania, Agosti 1, 2025. (Xinhua/Emmanuel Herman) |
Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania amezindua rasmi Kituo cha Biashara na Usafirishaji cha Afrika Mashariki (EACLC), kilichojengwa na kampuni ya China ya EACLC Ltd.
Akizungumza mjini Dar es salaam kwenye hafla ya uzinduzi, Rais Samia amekitaja kituo hicho chenye thamani ya dola za Marekani milioni 170, kuwa ni kitega uchumi kikuu kinacholenga kuimarisha uhusiano wa kibiashara na kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na China.
Mwenyekiti wa kituo hicho Bibi Wang Xiangyun, amesema kwa sasa kituo hicho chenye ukubwa wa zaidi ya mita za mraba 75,000 na maduka 2,060, ndicho kituo kikubwa zaidi cha biashara na usafirishaji wa bidhaa nchini Tanzania.
Alisema kutokana na kuunganishwa na maghala, ofisi ya idara ya forodha, biashara ya mtandaoni, idara za fedha, na usafirishaji nje, kituo hicho kinatarajiwa kupunguza gharama za biashara za kikanda kwa asilimia 30, kuleta zaidi ya ajira 50,000 za ndani, na kuleta mapato makubwa ya ushuru kusaidia maendeleo ya nchi . Pia ameutaja mradi huu kuwa ni matokeo ya ushirikiano kati ya China na Afrika, kupitia Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika.
Kwenye halfa hiyo Balozi wa China nchini Tanzania Bibi Chen Mingjian, amesema Tanzania inaendelea kuvutia idadi kubwa ya makampuni za China, na kuutaja mradi huu kuwa ni mfano bora wa kasi hiyo nzuri.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma